Kwa RC, KKKT na makanisa mengine
Simamia Jumuiya yako kwa uwazi, usahihi na urahisi.
Jumuiya.app inawasaidia viongozi wa Jumuiya ndogo ndogo kusimamia Kaya, Wana Jumuiya, Uongozi, Michango, Malipo, Risiti na Ripoti — mahali pamoja, kwa usalama.
Tayari una akaunti? Login
Kila kitu ambacho Jumuiya inahitaji
Kaya na Wana Kaya
Kila Kaya inatambulika kwa jina kamili la Mkuu wa Kaya. Historia ya wanakaya inahifadhiwa.
Wana Jumuiya
Sajili wanachama, uhusiano wao na Mkuu wa Kaya, Namba ya Ahadi na hali ya uanachama.
Uongozi na Ruhusa
Mwenyekiti, Katibu, Mtunza Hazina na vyeo vingine — kila mmoja na ruhusa zake.
Michango
Ada ya mwezi, harambee, michango maalumu — yenye au bila kiasi kinachotarajiwa.
Vitabu vya Michango
Fungua na funga vitabu kwa kipindi. Kitabu kilichofungwa hakipokei malipo mapya.
Malipo na Risiti
Rekodi malipo ya Cash, M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money, HaloPesa na Bank. Toa risiti papo hapo.
Ripoti
Makusanyo kwa tarehe, Kaya, mchango, njia ya malipo na salio — pakua CSV, Excel au PDF.
Registration links salama
Wanachama wajisajili wenyewe kupitia link inayoisha muda, kisha viongozi waidhinishe.
Faragha na Usalama
Kila Jumuiya ina nafasi yake binafsi. Taarifa zako haziwezi kuonekana na Jumuiya nyingine.
Anza kwa hatua tatu
- HATUA 1
Sajili Jumuiya
Chagua kanisa lako, jaza taarifa za Jumuiya, na uwe Mwenyekiti wa akaunti.
- HATUA 2
Ongeza Kaya na viongozi
Sajili Kaya na wanachama, au tuma registration link. Teua Katibu na Mtunza Hazina.
- HATUA 3
Simamia michango
Fungua kitabu cha mchango, rekodi malipo, toa risiti na pata ripoti sahihi.
Uko tayari kuanza?
Sajili Jumuiya yako leo na uanze kusimamia Kaya na michango kwa uwazi.
Sajili Jumuiya