Ruka hadi maudhui
Jumuiya.app

Huduma za Jumuiya.app

Kila kipengele kimeundwa kwa ajili ya Jumuiya ndogo ndogo za Kikristo Tanzania.

Kaya

  • Kila Kaya inaonyeshwa kwa jina kamili la Mkuu wa Kaya - bila "Kaya la/ya".
  • Mkuu wa Kaya anaweza kuwa Baba, Mama, Mlezi au mwakilishi mwingine.
  • Historia ya Wakuu wa Kaya na wanakaya huhifadhiwa daima.
  • Hali ya Ndoa ya Kikristo inarekodiwa kando na hali ya ndoa ya kawaida.

Wana Jumuiya

  • Taarifa kamili: jina, jinsia, tarehe ya kuzaliwa, simu, email, uhusiano.
  • Kuhamisha mwanachama kwenda Kaya nyingine bila kupoteza historia.
  • Hali: Inatumika, Hatumiki, Amehama, Amefariki, Imehifadhiwa.
  • Tafuta, chuja na pakua orodha (kwa ruhusa).

Uongozi na Ruhusa

  • Vyeo: Mwenyekiti, Mwenyekiti Msaidizi, Katibu, Mtunza Hazina - na vyeo vipya.
  • Cheo ni tofauti na ruhusa za mfumo.
  • Mfumo unazuia kuondoa msimamizi wa mwisho.

Michango na Vitabu

  • Michango inayoendelea, yenye tarehe ya mwisho, ya mara moja na inayojirudia.
  • Michango ya hiari haihesabiwi kama deni.
  • Vitabu vya kipindi (mfano mwaka 2027) vinavyofunguliwa na kufungwa.
  • Kufungua upya kitabu kunahitaji ruhusa maalumu na sababu, na kunarekodiwa.

Malipo na Risiti

  • Kila malipo ni muamala wake, wenye namba ya risiti ya kipekee.
  • Malipo ya sehemu (partial) na malipo mengi kwa mchango mmoja.
  • Malipo hayafutwi - hubatilishwa kwa sababu na kumbukumbu.
  • Risiti za kuchapisha na PDF.

Ripoti

  • Makusanyo kwa tarehe, mchango, Kaya, mwanachama na njia ya malipo.
  • Salio lililobaki, muhtasari wa mwezi na mwaka.
  • Ripoti ya kufunga kitabu na malipo yaliyobatilishwa.
  • CSV, Excel na PDF.