Sera ya Faragha
Imesasishwa: 12/10/2026
1. Taarifa tunazokusanya
Tunakusanya taarifa zinazowekwa na viongozi wa Jumuiya na wanachama: majina, namba za simu, email, taarifa za Kaya, uhusiano wa kifamilia, hali ya ndoa ya Kikristo (kwa hiari), na kumbukumbu za michango na malipo.
2. Matumizi ya taarifa
- Kuwezesha Jumuiya kusimamia Kaya, wanachama, uongozi na michango.
- Kutoa risiti, ripoti na notifications zinazohusiana na Jumuiya.
- Kulinda usalama wa mfumo na kuzuia matumizi mabaya.
3. Umiliki na utengano wa taarifa
Taarifa za kila Jumuiya ni mali ya Jumuiya husika. Jumuiya moja haiwezi kuona taarifa za Jumuiya nyingine. Wafanyakazi wa Jumuiya.app wanapata taarifa binafsi pale tu inapohitajika kwa support, kwa ruhusa maalumu, na hatua hizo zinarekodiwa.
4. Kushirikisha wengine
Hatuuzi taarifa zako. Tunaweza kutumia watoa huduma (mfano huduma za email au hosting) chini ya makubaliano ya usiri.
5. Usalama
Tunatumia HTTPS, password zilizofichwa (hashed), ruhusa kwa kila kiongozi, na kumbukumbu za ukaguzi (audit log) kwa hatua muhimu.
6. Muda wa kuhifadhi
Kumbukumbu za fedha huhifadhiwa kwa muda unaohitajika kwa uwajibikaji. Jumuiya ikifunga akaunti, inaweza kuomba nakala ya taarifa zake kabla ya kufutwa kulingana na sheria.
7. Haki zako
Una haki ya kuomba kuona, kusahihisha au kufuta taarifa zako kupitia viongozi wa Jumuiya yako au support. Tunazingatia Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Tanzania (2022).
8. Mawasiliano
Kwa maswali kuhusu faragha: [email protected].