Ruka hadi maudhui
Jumuiya.app

Vigezo na Masharti

Imesasishwa: 12/10/2026

1. Kukubali masharti

Kwa kusajili Jumuiya au kutumia Jumuiya.app, unakubali masharti haya kwa niaba yako na kwa niaba ya Jumuiya unayoiwakilisha.

2. Akaunti na viongozi

Mwenyekiti anawajibika kwa akaunti ya Jumuiya, ikiwemo kuwapa viongozi wengine access na ruhusa. Hifadhi password yako kwa siri.

3. Usahihi wa taarifa

Jumuiya inawajibika kwa usahihi wa taarifa za Kaya, wanachama na malipo inazorekodi. Jumuiya.app inarekodi malipo yaliyowekwa na viongozi; haithibitishi moja kwa moja miamala ya mitandao ya simu isipokuwa huduma hiyo itakapotangazwa rasmi.

4. Ridhaa ya wanachama

Viongozi wanapaswa kupata ridhaa ya wanachama kabla ya kuweka taarifa zao binafsi, na kuzitumia kwa shughuli za Jumuiya pekee.

5. Mipango na malipo ya huduma

Baadhi ya huduma zinahitaji mpango wa kulipia. Malipo ya mpango ni tofauti na michango ya wanachama. Usipolipia baada ya kipindi cha neema, akaunti inaweza kuwekwa katika hali ya kusoma tu; taarifa hazifutwi.

6. Matumizi yasiyoruhusiwa

Ni marufuku kutumia mfumo kwa udanganyifu, kujaribu kupata taarifa za Jumuiya nyingine, au kuhatarisha usalama wa mfumo.

7. Kusimamishwa kwa akaunti

Jumuiya.app inaweza kusimamisha akaunti inayokiuka masharti haya. Taarifa huhifadhiwa wakati wa kusimamishwa.

8. Mabadiliko

Tunaweza kubadilisha masharti haya. Mabadiliko makubwa yatatangazwa ndani ya mfumo.