Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Je, Jumuiya nyingine zinaweza kuona taarifa zetu?
Hapana. Kila Jumuiya ina nafasi yake binafsi. Mfumo unazuia kuona taarifa za Jumuiya nyingine katika kila ukurasa, ripoti, export na API.
Kwa nini Kaya inaitwa kwa jina la mtu?
Kaya inatambulika kwa jina kamili la Mkuu wa Kaya, mfano "John Mwakalinga". Mkuu akibadilika, jina la Kaya linabadilika pia bila kupoteza historia ya malipo.
Je, Mkuu wa Kaya lazima awe Baba?
Hapana. Anaweza kuwa Mama, Mlezi au mwakilishi mwingine. Kaya za wajane, wagane na wazazi pekee zinakubalika kikamilifu.
Je, malipo ya M-Pesa yanathibitishwa moja kwa moja?
Kwa sasa malipo yote yanarekodiwa na viongozi (manual). Unaweza kuweka namba ya muamala ya M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money au HaloPesa kama kumbukumbu, na kiongozi mwenye ruhusa anayathibitisha.
Tukikosea kurekodi malipo tunafanyaje?
Malipo hayafutwi. Kiongozi mwenye ruhusa anayabatilisha kwa kuandika sababu, au anafanya marekebisho yanayotengeneza muamala mpya. Kila hatua inarekodiwa.
Kitabu cha mchango ni nini?
Ni kipindi cha mchango, mfano Ada ya mwezi kwa mwaka 2027. Kitabu kikifungwa hakipokei malipo mapya hadi kifunguliwe upya kwa idhini.
Wanachama wanajisajili vipi?
Viongozi wanatengeneza registration link salama inayoisha muda (siku 7 kwa kawaida) na kuituma WhatsApp au email. Maombi yanaidhinishwa na viongozi kabla ya kuwa rasmi.
Kuna app ya simu?
Kwa sasa Jumuiya.app inafanya kazi vizuri kwenye browser ya simu. App za Android na iOS zinaandaliwa.